SKUKUU YA MT.YOSEFU KATIKA JIMBO KUU KATOLIKI DODOMA

Tukio kubwa lilofanyika tarehe !9-03-2022 katika Nyumba ya malezi huko Miyuji,ambalo limewakutanisha wanaume wakatoliki(UWAKA) na Makamo wa Askofu Padri Onesmo Wissi na kuhudhuriwa na Mapadre kutoka Parokia mbalimbali,pamoja na watawa mbalimbali na wanawake wakatoliki.Katika tukio hilo Padri Joseph Mponde Kazikunema alitoa mrejesho wa mapato na matumizi yote yaliyofanyika katika ukarabati wa nyumba ya malezi.Pia Makamo wa Askofu alizindua mfumo wa kidigital wa wanaume wakatoliki.

Picha hapo chini ni Makamo wa Askofu wakiwa katika picha ya pamoja na Madekano,Watawa na Mapadre