KUBARIKI NA KUZINDUA JENGO LA ROMA COMPLEX

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma Mhashamu Beatis Michael Kinyaiya-OFM Cap, Siku ya Jumamosi Tarehe 19/02/2022,amebariki na kuzindua Jengo la Kitega Uchumi la Jimbo linaloitwa Roma Complex,ambapo tukio hilo limeambatana na Ibada ya Misa Takatifu.

 

Misa hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Jengo hilo  imeadhimishwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es salaam Mhashamu Yuda Thadeus Ruwai'chi OFM Cap,pamoja na Askofu Msaidizi wa Jimbo hilo Mhashamu Stephano Lameck Musomba-OSA.

 

Aidha Misa hiyo Takatifu ya kubariki na kuzindua Jengo la Kitega Uchumi la Jimbo, imehudhuriwa na Makamu wa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma Padre Onesmo Andrea Wissi,Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Padre Chesco Peter Msaga-C.PP.S, Katibu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma Padre Justine Fentu,Katibu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es salaam Padre Vicent Mpwaji,Madekano,Maparoko, Mapadre,Watawa na Viongozi wa Kamati Tendaji ya Halmashari ya Walei Jimbo na Parokia mbalimbali za Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma.