MISA YA KUBARIKI MAFUTA YA KRISMA MWAKA 2022

Askofu Mkuu Beatus Kinyaiya wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma,siku ya leo Jumanne ya Tarehe 12?04/2022 ameongoza Ibada ya misa Takatifu ya kubariki Mafuta ya Krisma,katika Parokia ya Kanisa Kuu la Kiaskofu la Mt. Paulo wa Msalaba.

Mafuta hayo ya Krisma ambayo hutumika kwa Wakatukumeni,Wagonjwa na kumuweka Krelo katika Daraja Takatifu la Upadre au Uaskofu.

Aidha katika Misa hii,tulishuhudia Mapadre wote wa Jimbo na Mashirika wakirudia viapo au ahadi za utii kwa Askofu.

Pia katika tukio lingine tumeshudia viapo vya viongozi wa Kanda wa Jimbo Kuu yaani Dodoma,Kondoa na Singida.